IMEELEZWA kuwa baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja ambao una masharti mazito amepanga kuanza kushusha rugu kwa wachezaji wake wote waliomzingua msimu huu.
Aussems ambaye mkataba wake mpya umeeleza kuwa anatakiwa kuipeleka timu hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, kutetea kombe la Ligi Kuu Bara, Kubeba kombe la SportPesa, kubeba kombe la Mapinduzi na kufika sehemu nzuri kwenye michuano ya FA ameanza kuwapigia hesabu za kuwaengua wachezaji 10.
Wachezaji ambao wanahusishwa kwa sasa ni hawa hapa:-Zana Coulibary
ambaye alisajiliwa dirisha dogo kubeba mikoba ya Shomari Kapombe inasemekana bado anapaya kwenye nafasi hiyo.
Asante Kwasi
hajawa na msimu mzuri kutokana na majeruhi licha ya kuwa na uwezo kila anapopata nafasi inasemekana kwamba atatolewa kwa mkopo kwa kuwa mkataba wake bado haujaisha mpaka mwezi Augosti.
Haruna Niyonzima
Bonge moja ya kiungo ila kiburi na jeuri huenda vikamponza kuachwa na Mbelgiji wa Simba.
Nicholaus Gyan
Hajawa kwenye ubora wake msimu huu na amekuwa akikosa nafasi kikosi cha kwanza hivyo njia yake huenda ikawa nyeupe.
Juuko Murshid
Licha ya kuwa tegemeo ndani ya kikosi cha Timu ya Taifa cha Uganda imeelezwa kuwa kiburi chake ndani ya uwanja kinamfanya asiive chungu kimoja na mr Uchebe.
Paul Bukaba
Mpambanaji akiwa ndani ya uwanja ila bado hajamkosha mbelgiji huyo hivyo rugu huenda likamshukia msimu ujao.
Salim Mbonde
Msimu huu hajacheza hata mchezo mmoja kutokana na kuumwa muda mrefu. Hatakuwa na nafasi ndani ya kikosi cha mabingwa hao msimu ujao.
Mohamedd Rashid
Yupo kwa mkopo KMC ila hana nafasi ya kurejea ndani ya kikosi cha Simba msimu ujao.
Adam Salamba
Msimu huu haujawa bora kwake kutokana na kushindwa kuonyesha cheche zake alizokuwa nazo Lipuli, bado Aussems anampigia hesabu kumpa mkono wa kwa heri na huenda akatolewa kwa mkopo.
Pascal Wawa
Amecheza jumla ya michezo 21 ndani ya Simba mpaka sasa, yupo vizuri akiwa uwanjani ila bado mbinu zake hazijamkosha mbelgiji huyo wa Simba.
Haruna haondoki, Kifupi ni kwamba wachezaji wa kigeni wa 4 lazima waondoke! Wa ndani labda wa 5 ukijumlisha wa mkopo na watakao achwa kabisa!
ReplyDelete