May 9, 2019



Benchi la ufundi la Azam limewaweka pembeni wapinzani wao Lipuli FC ambao watacheza nao fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kisha kuamua kudili na mechi zao za Ligi Kuu Bara.


Lipuli FC juzi Jumatatu waliwafuata Azam FC kwenye hatua ya fainali ya Kombe la  Shirikisho baada ya kuwafunga Yanga kwa mabao 2-0. Mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Samora, Iringa.


Azam na Lipuli FC ndizo zitacheza fainali ambapo bingwa wa kombe hilo atajikatia nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, mechi hiyo itapigwa Juni Mosi, Uwanja wa Ilulu, Lindi.


Mratibu wa Azam FC, Philipo Alando amesema kuwa kwa sasa hawana mawazo juu ya fainali ya FA  badala yake wanapambana kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mechi zao za ligi kuu ambazo wanacheza kwa sasa.



“Ninadhani Lipuli sio wageni kwetu, tumeshacheza nao huko. Walimu watawapa maelekezo wachezaji juu ya nini cha kufanya, kwa sasa bado tuna mechi za ligi ambazo tunacheza, fainali bado iko mbali,” alisema Alando.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic