May 9, 2019


Kiungo mjanja-mjanja katika klabu ya Yanga, Feisal Salum 'Toto' anamaliza mkataba wake wa mwaka wa kwanza ndani ya kikosi cha timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Wakati akiwa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja, taarifa zinaeleza kuwa tayari ameshaanza kufuatiliwa na timu kadhaa za kimataifa ikiwemo Uingereza.

Taarifa za ndani ambazo tumezipata zinasema Toto ameanza kuwindwa na klabu kadhaa kutoka Uingereza japo mtoa taarifa hajataja kuweka wazi ni zipi.

Uwepo wa taarifa hizo umeanza kuumizwa vichwa viongozi wa Yanga kwa kujua namna gani wanaweza kumbakisha klabuni kwao kutokana na mchango wake.

Mpaka sasa kumekuwa na mazungumzo mengine ya kuanza kuongeza mkataba ili kuhakikisha anabakia Jangwani lakini yakifeli kuna hatihati ya mchezaji huyo kusalia.


1 COMMENTS:

  1. Sijuhi kwa undani lakini nahisi kama dogo anakuja #SIMBA SPORTS CLUB

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic