May 9, 2019


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya yanga umethibitisha kuwa hautapata huduma ya mchezaji wake Ibrahim Ajibu kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United ya Musoma, huko Mara.

Kwa mujibu wa Mratibu wa timu, Hafidh Saleh, amesema Ajibu amesalia Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu kutokana na hali yake kiafya kuwa si nzuri.

Mchezaji huyo ambaye amekuwa sehemu ya mafanikio ndani Yanga haswa msimu wa raundi ya kwanza katika kuisaidia timu kupata matokeo amepatwa na malaria tena ikiwa ni wiki kadhaa tangu apone.

Ikumbukwe Ajibu hivi karibuni hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kutokana na kuugua malaria na kusababisha ashindwe kucheza mechi kwa takribani wiki mbili.

Tayari hivi sasa kikosi cha Yanga kipo mjini Musoma na kesho kitashuka dimbani kukipiga na Biashara kwenye Uwanja wa Karume.

Katika msimamo wa ligi Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 80 huku watani zao wa jadi Simba wapo kileleni wakiwa na alama 81 walizozifikisha jana kutokana na ushindi wa aina yake wa mabao 8-1 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

2 COMMENTS:

  1. Kila la heri chama langu.Sawa tumetolewa FA lakini tujitahidi tushinde mechi zote zilizo baki angalau tuwe mshindi wa pili.Tutakuwa tumekata tiketi ya kucheza Klabu bingwa Afrika.Ajibu yeye tumeshamzowea.

    ReplyDelete
  2. hamna hiyo ya kukata tiketi kwa kushika nafasi ya pili..Kuwa natasi ya pili bila kushinda FA cup inamaanisha Yanga kuendelea kwenda kwa Mkapa kushangilia time za nie zinazocheja na Simba!
    Mwaka 2020/21 endapo Yanga itakuwa nafasi ya pili bila kuchukua FA, itapata nafasi ya CAF, shukurani fadhila za Simba kwani mwaka huu wamefanya bidii na kufika mbali hadi Tanzania yetu kupewa nafasi nne

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic