May 25, 2019


KOCHA wa Singida United, Felix Minziro amesema kuwa kwa sasa anwaskilizia mabosi wake hao endapo watamuita mezani ili kujadili nae juu ya kuongeza mkataba kwani mpaka sasa bado hajajua hatma yake ndani ya kikosi hicho.

Minziro aliitwa na uongozi wa Singida United kuokoa jahazi baada ya makocha waliopewa timu kushindwa kuhimili mikikimikiki ya kikosi hicho hasa baada ya kuyumba kiuchumi.

"Nipo na Singida United napiga kazi ila hakuna majadiliano ya mkataba ambayo tumeyafanya kwa sasa kwani msimu unapomalizika nami mkataba wangu unamalizika, mpaka sasa bado sijazungumza na viongozi.

"Kwa sasa sifikirii sana kuhusu mkataba wangu lengo langu kuona nashinda mchezo wangu wa mwisho ugenini dhidi ya Coastal Union kisha mengine yatafuata," amesema Minziro.

Singida United ipo nafasi ya 11 imecheza michezo37 na ina pointi 45.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic