May 25, 2019


KOCHA wa Simba, Patrick Aussems leo amegoma kuzungumza kuhusu mechi yake dhidi ya Biashara United iliyochezwa uwanja wa Taifa na kikosi chake kuambulia sare ya kufungana bao 1-1.

Aussems amesema kuwa hawezi kuuzungumzia mchezo huo kwa kuwa hajaona kitu kilichotokea kiufundi kwani wachezaji walikwa wanacheza kwenye bwawa.

"Kuhusu mchezo samahani siwezi kuzungumzia chochote maana niliona wachezaji wanacheza kwenye bwawa sasa sijui nizungumzie nini hivyo mtanisamehe leo, labda kama kutakuwa na jambo lingine nje ya mchezo wa leo," amesema Aussems.

Simba na Biashara leo zimecheza mchezo wa pili kwenye uwanja wa Taifa ambapo mchezo wa kwanza uliochezwa Karume Simba ilishinda mabao 2-0 na leo ilibidi wakabadhiwe kombe la ligi imeshindikana kutokana na udhuru wa mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kushindwa kufika hivyo watakabidhiwa Mei 28, uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic