May 25, 2019



KOCHA wa timu ya Biashara United, Amri Said amesema kuwa leo anaifunga timu ya Simba ili kujihakikishia nafasi ya kubaki ligi kuu kwa kuwatibulia sherehe yao ya kupewa ubingwa kwani kuna wachezaji wakali amewapata kwa ajili ya kuboresha safu ya ushambuliaji wa kikosi chake.

Biashara United ipo kwenye hatari ya kushuka daraja endapo itapoteza michezo yake miwili ya mwisho iliyobaki ambapo leo itaanza na Simba uwanja wa Taifa na itamaliza na Mbeya City Mei 28 uwanja wa Samora Iringa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Said amesema kuwa amepata wachezaji wazuri kutoka nchi ya Congo ambao wana uwezo mkubwa wa kucheza na kufunga wapo tayari kujiunga na Biashara msimu ujao endapo hatashuka daraja hivyo leo lazima apambane.

"Wachezaji nimewapata kutoka Congo ambao wana uwezo mkubwa hivyo nimewaambia wasubiri kwanza nipambane na timu ibaki kwenye ligi kisha msimu ujao nitawasajili moja kwa moja kwenye kikosi changu ambacho kitatisha nikiwapata.

"Ninachotakiwa kufanya kwa sasa ni kushinda mechi zote ikiwa ni pamoja na hii dhidi ya Simba nitakachofanya ni kutibua mipango yao kwa wachezaji wangu kupata pointi tatu muhimu, ninawaheshimu Simba ni timu nzuri ila kwa sasa hamna namna nami ni lazima nionyeshe uwezo," amesema Said. 

Biashara United ya Mara imepanda daraja msimu huu imecheza jumla ya michezo 36 ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi zake 43 kibindoni leo itacheza na Simba ambayo itakabidhiwa kombe lake la msimu huu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic