May 14, 2019


Bao pekee la Papy Tshishimbi mnamo dakika ya 16 kunaki kipindi cha kwanza limeipa Yanga alama tatu muhimu katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting iliyopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.

Yanga ilikuwa ikikipiga na timu hiyo ya jeshi ambapo matokeo yameifanya kurejea kileleni kwa kufikisha jumla ya alama 83 nyuma ya watani zao wa jadi Simba walio na 82.

Katika mchezo wa leo Yanga ilitawala zaidi kipindi cha kwanza licha ya kufunga bao moja safu yake ya ushambuliaji haikuwa makini kwa kufanya baadhi ya makosa.

Kuelekea mwisho kunako kipindi cha kwanza kiungo wa Yanga Rafael Daud alishindwa kufunga bao baada ya kupaisha mpira langoni mwa Ruvu Shootinga akiwa yeye na kipa, tukio lililowaacha hoi mashabiki wengi uwanjani.

Na kunako kipindi cha pili Ruvu Shooting walikuwa juu kulisakama lango la Yanga wakitawala mchezo lakini uimara wa beki ya Yanga ulikuwa makini katika kulinda lango lao.

Mpaka dakika 90 za mchezo huo zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa ba0 moja na Ruvu wakiwa na sifuri.

Msimamo wa ligi unaonesha Yanga waliosalia na mechi mbili wapo kileleni wakiwa na alama 83 huku Simba akishika nafasi ya pili na alama zake 81 huku Azam aliye nafasi ya tatu akiwa na alama 69.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic