May 31, 2019


YANGA wamejiwekea msimamo kwamba wachezaji wote wazawa kila mmoja mkwanja wake wa usajili usizidi Sh.Mil 30 lakini kuna baadhi wanaweza kuwafi kiria kidoogo.

Gadiel Michael ni mmoja wao. Sasa wakubwa wakamuendea hewani wakamwambia ; “njoo umwage wino kuna mil 40 hapa.”

Gadiel akawaambia “niongezeeni kidogo kwavile mara ya kwanza mlinipa Mil 30 wakubwa” Yanga wakamwambia hamna noma njoo fasta tuyajenge, Gadiel akawasha gari kuwafuata viongozi wakati yuko njiani akamtumia meseji wakala wake kwamba; “Mimi ndio naenda kuwasikilizia jamaa.”

Meneja akamuendea hewani fasta akamwambia ; “Wee…usiende rudi, ukiwapa nafasi ya uso kwa uso watakushinda.”

Mchezaji akageukia njiani Yanga wakasubiri weee… wakaishia kumsainisha Papy Tshishimbi. Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra imezipata ni kwamba mpaka jana Gadiel alikuwa anakomaa na Yanga akitaka wampe Sh.60Mil kwa mkataba wa miaka miwili.

Mchezaji huyo wa zamani wa Azam anatajwa pia kuwindwa na Simba na mashabiki wametengeneza jezi ya mitandaoni wakiwarusha roho Yanga. Gadiel ni kati ya wachezaji 15 ambao mikataba yao imemalizika na Zahera amesisitiza kwamba wanaweza kuondoka tu kama akiamua vinginevyo kwavile ana wachezaji kibao.

3 COMMENTS:

  1. Huyu ni mbadala wa Kwasi pale Simba, kwa MO atakula m80, Majembe ya nje yawe wale wenye uwezo kweli kweli ila kama wapo wa ndani ni bora wachukue hizo nafasi. Gadiel namkubali sio siri.......

    ReplyDelete
  2. Bado Simba haijatatua tatizo la mabeki wa maana.....beki #3 anatakiwa mtu mwenye uwezo na Uzoefu wa CAF...hawa mabeki (Gadiel & Tshbalala) hawawezi kuzuia forward kali za Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca walioenda juu na wenye kushiba na wenye kasi....tofauti za uchezaji kwa Gadiel na Tshabalala hakuna... NARUDIA tena ni mara mia (100×) Simba tumsajili WALUSIMBI NAMBA 3 KULIKO GADIELI....TUNZA KUMBUKUMBU YA COMMENT HII MTAKUJA KUNIAMBIA.......Simba tunataka mabeki wazoefu na CAF CL....sio mabeki wa kuwazuia lipuli, Ndanda, na alliance!!....huko sie tumeshatoka.....tunadeal jinsi ya kushindana na Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca haswa mechi za ugenini....kwahiyo akina Gadieli hawatatusaidia kitu....hakuna tofauti na Tshabalala!

    ReplyDelete
  3. Bado Simba haijatatua tatizo la mabeki wa maana.....beki #3 anatakiwa mtu mwenye uwezo na Uzoefu wa CAF...hawa mabeki (Gadiel & Tshbalala) hawawezi kuzuia forward kali za Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca walioenda juu na wenye kushiba na wenye kasi....tofauti za uchezaji kwa Gadiel na Tshabalala hakuna... NARUDIA tena ni mara mia (100×) Simba tumsajili WALUSIMBI NAMBA 3 KULIKO GADIELI....TUNZA KUMBUKUMBU YA COMMENT HII MTAKUJA KUNIAMBIA.......Simba tunataka mabeki wazoefu na CAF CL....sio mabeki wa kuwazuia lipuli, Ndanda, na alliance!!....huko sie tumeshatoka.....tunadeal jinsi ya kushindana na Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca haswa mechi za ugenini....kwahiyo akina Gadieli hawatatusaidia kitu....hakuna tofauti na Tshabalala!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic