May 26, 2019

KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa hasira zake kwa sasa ni mchezo wa mwisho dhidi ya Mbao utakaopigwa Mei, uwanja wa Nyamagana.

 Kagera Sugar ilipoteza mchezo wake jana mbele ya JKT Tanzania mchezo uliochezwa uwanja wa JMK, kwa mabao 2-0 yote yalifungwa na Hassan Mwatelema.

Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa kwa sasa hana cha kufikiria zaidi ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mbao .

"Nimepoteza mchezo sijapoteza matumaini, kazi yangu inayofuata ni dhidi ya Mbao hivyo tutapambana ili kupata matokeo kwenye mchezo wetu wa mwisho," amesema.

Kagera Sugar imecheza jumla ya michezo 37 imejikusanyia pointi 43 inashika nafasi ya 17 mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mbao FC ndio utakaoamua hatma yao kubaki kwenye ligi ama kushuka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic