May 26, 2019


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hauna presha na wachezaji ambao utawafanyia usajili msimu ujao kwani tayari kazi hiyo wamemuachia kocha mkuu, Mwinyi Zahera ambaye anashughulikia mafaili yote ya wachezaji.

Yanga mpaka sasa wachezaji wake 16 wa kikosi cha kwanza wanamaliza mikataba yao msimu huu hivyo kinachosubiriwa ni kuwaongezea mkataba wale ambao watakidhi vigezo vya kocha.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa kwa sasa hawashughuliki na masuala ya usajili kazi hiyo wamemuachia Zahera.

"Kuhusu usajili sisi tupo vizuri kwanza tunaanza na wachezaji ambao mikataba yao inamalizika na wameonyesha kazi kubwa na kocha akawakubali hivyo hatma yao ipo mikononi mwa Zahera," amesema Mwakalebela.

Wachezaji ambao inaelezwa kwamba mikataba yao inakwisha msimu huu ni pamoja na Ramadhani Kabwili,Haji Mwinyi, Pato Ngonyani, Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Said Juma Makapu, Matheo Anthony, Thabani Kamusoko, Raphael Daudi, Pius Buswita, Juma Mahadhi, Baruani Akilimali, Amissi Tambwe, Haruna Moshi.

3 COMMENTS:

  1. Hao wanigeria (Victor Patrick Okpan na Shehu) ni matapeli mchezaji wa maana labda huyo mguinea kwani alicheza ligi ulaya na anaonekana kwenye youtube hao wengine (ivory coast na nigeria hamna kitu mtapigwa na mtakuwa mmeliwa)

    ReplyDelete
  2. Ina maana Yanga haina mshambualiaji hata mmoja kwa sasa nilifikiri wataanza usajili wa strikers 4 lakini kimya!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tulia wewe subiri muda ufike

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic