May 9, 2019


Baada ya kupanda katika msimamo wa Ligi Kuu Bara mpaka nafasi ya kwanza, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema malengo yao kwa sasa ni kutetea ubingwa wa ligi.

Aussems amesema hayo kutokana na Simba kuwa kileleni ikiwa na alama 81 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga walio na 80 mpaka sasa.

Kocha huyo ameeleza kwa sasa anaangalia zaidi mechi zake zijazo haswa kuelekea mechi ijayo na Kagera Sugar.

"Lengo kubwa ni kutetea ubingwa na sasa tunaongoza ligi tukiwa na michezo mitatu nyuma ya wapinzani wetu.

"Mimi naangalia zaidi timu yangu na mpinzani wangu ajae Kagera, timu zingine sijali."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic