May 9, 2019


Kikosi cha Yanga kinashuka dimbani kesho Karume Stadium mjini Musoma, Mara kucheza na Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Yanga inaenda kukipiga na Biashara ikiwa imeshushwa nafasi ya pili kunako msimamo wa ligi ikiwa na alama 80 dhidi ya 81 za Simba.

Kuelekea mchezo huo Yanga wamedhamiria kwa dhati kupata matokeo ili kushinda waweze kurejea tena kwenye nafasi ya kwanza.

Kwa utofauti wa alama uliopo Yanga ikishinda mchezo wa kesho itapanda tena mpaka nafasi ya kwanza na itafikisha alama 83 na kuwaacha Simba kwa alama mbili.

Hata hivyo Yanga itakosa huduma ya mchezaji wake Ibrahim Ajibu ambaye ameachwa Dar es Salaam kutokana na kuwa majeruhi.

Yanga itaweza kurejea kileleni endapo itashinda mchezo wa kesho na Simba iende sare ama ipoteze dhidi ya Kagera Sugar.

4 COMMENTS:

  1. Majruhi gani bwana kwanini hamsemi kweli

    ReplyDelete
  2. Kwani simba kesho hachezi?Yanga itaing'oaje Simba kwa mfano!

    ReplyDelete
  3. Wasahau kabisa,kama walishindwa kupiga picha ya kuongoza juzi ndo basi tena ivo

    ReplyDelete
  4. WEWE KWELI SHABIKI. TIMU ZOTE 2 YANGA NA SIMBA ZINACHEZA KESHO. SIMBA ATASHINDA NA YANGA ATASHINDA. SASA YANGA ATAKUWA NA POINTI 83 NA SIMBA 84. BADO SIMBA ATAONGOZA. TATIZO WEWEUNAOMBEA YANGA TU NDIO ASHINDE SIMBA ASHINDWE. MUNGU SI ASUMANI.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic