MAFURIKO DAR, WANANCHI WALIA – VIDEO
MVUA zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam kwa wiki nzima mfululizo zimesababisha mafuriko makubwa katika Bonde la Mto Msimbazi, maeneo ya Daraja la Kigogo Wilaya ya Ilala, Jangwani, Vingunguti na maeneo mengine ambayo Mto Msimbazi unapita.
Hali hiyo imezua taharuki miongoni mwa wakazi wa maeneo ya kandokando na mto huo lakini hakuna nyumba iliyoripotiwa kubomolewa na mvua hizo, watu kujeruhiwa wala kufa ama familia kupoteza makazi yake.
Hata hivyo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar zimeshindwa kupitika kutokana na wingi wa maji na tope, jambo ambalo limesababisha magari na vyombo vingine vya moto kushindwa kupita kirahisi.
Watu walioathirika zaidi kutokana na mafuriko hayo ni watu waliojenga mabondeni, hasa maeneo ya Jangwani, na bonde lote la mto Msimbazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment