May 14, 2019


Ofisa Habari wa Ruvu Shooting ameshangazwa na uwezo wa Yanga waliounesha dhidi yao katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo limewekwa kimiani na Papy Tshishimbi mnamo dakika ya 16 ya mchezo na kuweza kuwapa mabingwa hao wa kihistoria alama tatu wakikwea kileleni.

Licha ya ushindi huo, Bwire amesema Yanga wamecheza kwa kuonesha uwezo mdogo zaidi tofauti na wao ambao wamekuwa wakicheza kama Barcelona ya Spain.

"Licha ya kutufunga lakini nimeshangazwa na uwezo waliouonesha Yanga kwenye mchezo wa leo.

"Ni uwezo mdogo na wa kawaida mno ukiachana na sisi tuliokuwa tunacheza kama FC. Barcelona, walikuwa wanacheza kama JUDO."

2 COMMENTS:

  1. Haya Mzee tumekusikia na tumekuzoea.Asante.

    ReplyDelete
  2. Shukuru hilo goli moja,ungetia kichwa kwa Simba ungepigwa saba,mchana kweupe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic