May 26, 2019


MASHABIKI kibao wa Simba jana jioni walitinga katika Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi dhidi ya Biashara huku kichwani wakiwa wamevaa kofia helmeti za Bodaboda.

Tukio hilo lilijiri katika mechi ambayo uwanja ulikuwa chepechepe kutokana na mvua lakini hata
Simba hawakupewa kombe lao kama walivyotarajia.


Mashabiki wa Simba wamefikia hatua hiyo ikiwa kama sehemu ya kusapoti kauli ya mwekezaji wao, Mohammed Dewji ‘Mo’ ambaye ameahidi kuwapatia wachezaji wa timu hiyo pikipiki kwaajili ya kufanya ujasiriamali.

Mbali na kuvaa helmeti mashabiki hao waliimba nyimbo mbalimbali za kumpongeza ‘Mo’ kwa kutoa ahadi hiyo; “Mjini foleni bodaboda inapenya.” Walisikika mashabiki hao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic