May 26, 2019


KIUNGO mkabaji wa Yanga, Papy Tshishimbi amefunguka kuwa ameongeza mkataba Yanga sasa mambo yatakuwa biyee na ataipa ubingwa msimu ujao.

Tshishimbi ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu bara kufuatia mkataba wa kwanza kumalizika alijiunga na timu hiyo akitokea Mbabane Swallows ya Eswatini.

Kiungo huyo raia wa DR Congo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba alijiunga na Yanga katika msimu wa mwaka 2018.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Tshishimbi alisema kuwa ana furaha ya kuongeza mkataba wa miaka miwili katika timu hiyo kwani malengo yake ni kutaka kuipa ubingwa wa msimu ujao.

Nina furaha ya kuweza kuongeza miaka miwili katika timu yangu, naamini Yanga ni timu bora tofauti na nilipokuwa nacheza awali. “Miaka miwili katika mkataba wangu nadhani nitafanya kilicho bora ili tushinde makombe nikiwa katika hii timu kubwa na hilo ndiyo lengo la kubaki kwangu,” alisema Tshishimbi.

2 COMMENTS:

  1. Ubingwa muusahau sana itabidi muungojee kutokana na Mnyama alivo hashikiki

    ReplyDelete
  2. Mnawazia ubingwa wa Bara, wakati wenzenu wanataka kufikia hatua ya fainali mwakani. Kweli tumetofautiana sana kimtazamo.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic