May 8, 2019


KOCHA Msaidizi wa Lipuli FC, Selemani Matola, amesema dharau za Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ndiyo sababu kubwa ya kupoteza mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), juzi Jumatatu.

Matola aliliambia Championi Jumatano kuwa, alimsikia Zahera akisema wameenda Iringa kuwaaibisha wenyeji wao kitu ambacho ilionekana ni dharau.

Aliongeza kuwa, baada ya kusikia kauli hiyo, alipania kuwafunga Yanga ili kukwepa aibu na dharau za Zahera ambaye alisema kwenye mchezo wa ligi walipocheza uwanjani hapo, walifungwa kwa kwa bahati.

“Mbali na vijana wangu kuahidiwa shilingi laki 5 kwa kila bao, bado tulijipanga kushinda ili kukwepa fedheha ya kuambiwa tumenunuliwa na Yanga.

“Lakini pia hakuna jambo ambalo lilitukwaza kama kusikia kocha mwenzangu akisema mchezo wa kwanza tulibahatisha na akisahau ubora wa vijana wangu ambao ndiyo chachu ya ushindi wetu huku akisema amekuja kutuaibisha,” alisema Matola.

Aliongeza kuwa; “Tulikuwa na nafasi ya kuwapiga mabao matano kutokana na kasi ambayo tulianza nayo kipindi cha kwanza na kipindi cha pili ila ndio hivyo tumeambulia mabao mawili.”

“Kwa Yanga ukiwabana mabeki na ukicheza kwa nidhamu ni rahisi kushinda hivyo hawakunipa kazi kuwamaliza, sasa kazi inayofuata ni dhidi ya Azam FC hakieleweki mpaka tubebe ubingwa,” alisema Matola.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Lipuli kutinga hatua ya fainali ya shirikisho ambapo bingwa wa michuano hii anaiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.

3 COMMENTS:

  1. Ukimuangalia Othmani khazi na kipindi chake cha kipenga cha mwisho basi utajua kumbe Yanga ndio timu inayobebwa na waamuzi. Na kushangaza masikini Simba wanaangushiwa jumba bovu kwa tuhuma feki.

    ReplyDelete
  2. Exactly, me pia niliangalia hicho kipindi ilionyesha ile match ambayo simba walipata 2 penalties zote zilikuwa halali kabisa hata muamuzi wa kati alifungiwa kimakosa, isipokuwa lineman mmoja ndo alishindwa kutafsiri sheria ya offside kwa Simba na KMC pia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic