May 10, 2019


DADA wa Diamond Platnumz, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ amesema katika maisha yake kamwe hawezi kuingilia malumbano ya mdogo wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anapoona hawako sawa.

Akizungumza na Amani, Darleen alisema kuwa siku zote yeye si mchangiaji kwenye tofauti za Diamond na Zari kwa sababu anaamini anaweza kufanya hivyo halafu siku wakipatana, akajikuta akikosa pa kuiweka sura yake.

“Sina tabia kabisa ya kuingilia ugomvi wa kaka yangu na wazazi wenziye, siyo Zari tu hata wengineo kwa hiyo hata kama kuna malumbano yao huwa nakaa kimya, naamini watayamaliza wenyewe mimi ni mtazamaji tu siku zote,” alisema

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic