May 31, 2019


Straika tegemo katika timu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji, Mbwana Samatta, amesema kuwa endapo atamaliza harakati za maisha yake ya soka atarejea Tanzania kuungana na Simba.

"Wachezaji wengi wakubwa wanapokaribia kustaafu soka hurudi kwenye klabu zao vya zamani ambavyo viliwatoa.

"Nilikuwa mchezaji wa Simba zamani, hata nitakaporudi baadaye nafikiri nafasi ya kwanza itakuwa kwa Simba kwa sababu niliwahi kuitumikia lakini kama watakuwa hawanitaki ndio nitaangalia sehemu nyingine.
.
"Kwa heshima yao kwa sababu niliwahi kuwa mchezaji wao kwa hiyo nafasi ya kwanza lazima itakuwa kwao."

TP Mazembe ya DR Congo ilimsajili Samatta akitokea Simba na alicheza kwa mafanikio makubwa na kuwapa ubingwa wa Afrika.

Baada ya hapo alianzisha safari maya ya maisha alipojiunga na KRC Genk ambayo pia amefanikiwa kuipa ubingwa.


1 COMMENTS:

  1. Wallahi tutakupokea Kwa maelfu ya mikono. Waswahili walisema mwenda tezi na homu hurejea ngamani. Old Is Gold, lakini bora usichelewe Sana urejee kuikimu misikiti yako mwanangu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic