May 31, 2019


NYOTA wawili wa Kagera Sugar, Ramadhan Kapera na Kassim Khamis wameonyesha dalili za kuihama timu hiyo itakayocheza Play off na Pamba huku Simba na Yanga zikitajwa kuonyesha nia ya kuwasajili washambuliaji
hao.

Kapera na Khamisi walikuwa msaada mkubwa katika klabu ya Kagera Sugar na kuwa mwiba mkali katika michezo mingi ya ligi kuu hasa ule wa Simba uliopigwa katika Uwanja wa Kaitaba ambapo wote walifunga bao moja moja na kuipa Kagera ushindi wa mabao 2-1.

Rafiki wa karibu na wachezaji hao, alisema wachezaji hao wanawindwa na timu nyingi zikiwemo Simba na Yanga na hali ilivyo wataachana na klabu hiyo katika wiki za karibuni.

“Unajua wale walianza kuwindwa kabla hata ligi haijafi ka mwishoni, timu nyingi sana zilionyesha nia ya kutaka kuwasajili hata hawa Simba na Yanga wameonekana kuwahitaji sana nafi kiri muda siyo mrefu wataondoka katika klabu hiyo,” alisema mtoa habari huyo.

5 COMMENTS:

  1. Mwenye hela ya hakika ndiye atayeula

    ReplyDelete
  2. we unaongelea usajili wa Simba Kama Nani. wenyetimu wanakwambia wataanza usajili wiki ijayo

    ReplyDelete
  3. Huu ujinga kumbe haujawahi kuishaga tu kule Simba...
    Hivi hao wanawasajili kwa sababu waliwafunga au ni kwa sababu wanawahitaji zaidi kuliko kawaida..??

    ReplyDelete
  4. Hawa wengine tuwe tunawaacha tu jamani, wakicheza na Simba wanacheza kwa kutumia nguvu zao zote walizonazo, wanakamia, lakini kwa uwezo wao wa kawaida hawapo hivyo.

    Hawa ndo wale tukiwaleta huku, wanacheza kwa uwezo wao wa kawaida, matokeo yake tunawaona hawaendani na uwezo wa timu kubwa. Lakini kumbe tumekosea kuwa-scout. Kule walitumia nguvu kuzidi kawaida ili waifunge Simba tu!. C mmeona wapo katika hali gani kwasasa?

    Kama wangekuwa ni wafungaji wazuri, wasingefikia hatua ya kuanza kuangali mpishano wa magoli ya kufungwa na kufunga ili wasishuke daraja. Wangekuwa na mabao mengi ambao hao Stand wasingeweza kfananishwa nao. TUWAACHE BHANA.

    ReplyDelete
  5. wote hawana uwezo wa kuchezea simba hao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic