May 26, 2019


KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa, Singida United wasahau habari za kuwatumia kama daraja la kubaki kwenye ligi msimu huu lazima waziache pointi tatu uwanja wa Mkwakwani kwa namna yoyote ile.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa wamejipanga kupata pointi tatu mbele ya Singida United  ili kumalizia malengo yao ya msimu huu.

"Tulianza ligi tukiwa na malengo makubwa mawili, kubaki ndani ya ligi ambalo limetimia na la pili ilikuwa ni kuhakikisha tunakuwa ndani ya 10 bora, sasa ni lazima yatimie.

"Tumetimiza la kwanza kubaki ndani ya ligi, bado kazi moja ya kubaki ndani ya 10 bora, ndugu zetu Singida United watatusamehe kwa kweli lazima tubaki na pointi tatu," amesema.

Coastal Union ipo nafasi ya 10 baada ya kucheza michezo 37 na ina pointi 47 inamaliza ligi kwa kucheza na Singida United ambao wanahitaji pointi moja kubaki kwenye ligi msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic