May 26, 2019


NYOTA wa kikosi cha Mwadui FC, Salim Aiyee amesema kuwa wana imani kubwa ya kubaki kwenye ligi msimu ujao kutokana na hesabu kuwabeba hasa kutokana na kujipanga vizuri kupata ushindi mbele ya Ndanda FC.

Mwadui FC Ipo nafasi ya 19 baada ya kucheza michezo 37 na imejikusanyia pointi 41, mchezo wake wa mwisho itamenyana na Ndanda FC iliyo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 48.

Akizungumza na Saleh Jembe, Aiyee amesema kuwa mchezo wao wa mwisho watatulia na kutumia vizuri uwanja wa nyumbani kupata matokeo chanya.

"Tupo kwenye hatari ya kushuka Daraja msimu ujao, sasa tutatumia mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Ndanda FC hivyo tunaimani ya kubeba pointi tatu ili kubaki kwenye ligi," amesema Aiyee.

Aiyee ametupia jumla ya mabao 17 msimu huu akiwa ni kinara kwenye timu yake kwa kupachika mabao na anashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa watupiaji TPL.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic