May 13, 2019


NEEMA imeanza! Hivyo ndivyo utakavyoweza kusema ni baada ya uongozi wa mpya wa Klabu ya Yanga kupata udhamini wa kwanza wa shilingi milioni 20 tangu uingie madarakani.

Uongozi huo mpya wa Yanga uliingia madarakani wikiendi iliyopita kwa Mshindo Msolla kushinda nafasi ya mwenyekiti huku makamu wake akiwa ni Fredrick Mwakalebela.

Kwa mujibu wa Championi Ijumaa mara baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Mwakalebela alisema udhamini huo walioupata ni sehemu ya ahadi zao walizozitoa katika kampeni zao za uchaguzi yeye pamoja na Msolla.

Mwakalebela alisema udhamini huo wameupata kutoka kwa mmoja wa wanachama wa timu hiyo, Yono Kevela kwa kushirikiana na washirika wake.

Aliongeza kuwa fedha hizo za udhamini zitatumika kwa ajili ya matayarisho ya michezo minne waliyoibakisha ya Ligi Kuu Bara ukiwemo wa jana Ijumaa dhidi ya Biashara United uliopigwa kwenye Uwanja wa Karume na Musoma.

“Udhamini huu tulioupata ni katika kutekeleza sehemu ya ahadi zetu tulizozitoa kabla ya uchaguzi tukiwa katika kampeni mimi pamoja na mwenyekiti wangu, Msolla.

“Hivyo, huu ni mwanzo wa kutafuta udhamini kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi nyingine, hivyo mengi yanakuja mazuri kwenye uongozi huu wetu mpya.

“Kwa kuanzia hizi fedha zilizopatikana za shilingi milioni 20 zitatumika katika michezo minne ya ligi tuliyoibakisha kwa ajili ya kuandaa timu kwa maana ya kuiweka timu katika kambi nzuri na usaļ¬ ri,” alisema Mwakalebela.

Kwa upande wake Kevela aliyejiondoa katika hatua za mwisho za kugombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo alisema:

“Nimefanikisha udhamini huu wa ili kuthibitisha kuvunjika kwa makundi na utimu unaokuwepo katika kipindi cha uchaguzi.

“Hivyo, niwaambie wagombea wengine walioshindwa katika nafasi ya kugombea katika uchaguzi wa Yanga kuungana na kufanya kazi na uongozi mpya ulioingia madarakani kama ilivyokuwa kwangu na kikubwa ni kuijenga Yanga,” alisema Kevela.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic