May 30, 2019


IMEEELEZWA kwamba uongozi wa Yanga umeanza mazungumzo na beki wa kikosi cha KMC, Ally Ally 'Mwarabu' ili kupata saini yake msimu ujao.

Mwarabu amekuwa kiongozi ndani ya KMC na kuifanya safu ya ulinzi kuwa kisiki kwani KMC imekuwa ni namba moja kwenye timu zilizotoa sare nyingi ikiwa imefanya hivyo mara 16 msimu huu.

Habari zimeelezwa kuwa Yanga tayari wamefikia sehemu nzuri ya maelewano na beki huyo ambaye ni mwepesi akiwa ndani ya uwanja.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa suala la usajili lipo mikononi mwa kocha mkuu, Mwinyi Zahera hivyo kama jina lake lipo litafanyiwa kazi.

"kama jina lake lipo kwenye orodha ya mwalimu inawezekana tukazungumza naye ila kwa sasa hakuna taarifa kamili," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Yanga fanyeni usajikwia makini lakini wachezaji waliowapitisha kayika kipindi kigumu muwaache kwa hesima wamefanya kazi ya kujitolea sana. Na sio mwisho wa mchango wao kumbukeni na mjifunze kwa dilunga.

    ReplyDelete
  2. Duh usajili unaoendelea mitaa ya Jangwani ni balaa hii inaitwa "Yanga Kubwa Kuliko" wengine wanaiita "Yanga Mabadiliko" au "Yanga Yenye Kasi Mpya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic