May 9, 2019


Wakati mabingwa wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara klabu ya Yanga wakiwa kwenye mchakato wa kumsajili mchezaji Jacques Tuyisenge kutoka Gor Mahia FC, imeelezwa kuwa AS Vita Club toka Congo nao wameanza kutaka saini ya mchezaji huyo.

Taarifa kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo, Patrick Gakumba, amesema tayari walishaongea na Yanga na aliwapa masharti ya kuhakikisha analipwa milioni 18 kwa mwezi.

Baada ya kutolewa kwa masharti hayo, mpaka sasa Yanga wameonekana kuwa kimya lakini vilevile zimekuja taarifa za Vita kutaka namba ya mchezaji huyo.

Vita ambao ni vinara wa Ligi Kuu Congo hivi sasa wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili Tuyisenge kutokana na ukubwa wa klabu yenyewe pamoja na kuwa na mpunga mwingi tofauti na Yanga,

Hii si mara ya kwanza kwa taarifa za mchezaji huyu kutajwa kutua Yanga lakini vilevile miezi kadhaa iliyopitwa Simba SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara nao walitajwa kutaka saini ya mchezaji huyo ila baadaye uongozi ukakanusha taarifa hizo.


4 COMMENTS:

  1. Zahera ni nyoka kampeleka mwenyewe huko!Tanzania hatutamsahau aliposambaza fitina eti timu yetu inapuliza dawa vyumba vya wachezaji wa timu ngeni

    ReplyDelete
  2. Mwenye kisu kikali ndio mlaji wa nyama.Zahera anamtaka Tuyisenge udi na uvumba ili kuimarisha safu ya ushambuliaji.Haiwezekani awe ndumila kuwili.

    ReplyDelete
  3. mtu anaheshimika katokana na maneno na vitendo vyake!Ni Zahera aliyepeleka kikosi cha Yanga B Zanzibar ili wanaocheza ligi kuu na watakaocheza Sports Pesa wapumzike kisha waendelee na mazoezi Dar!Eti ni mbinu za ubingwa!Na akatangaza kuwa atachukua makombe yote matatu, Mapinduzi, FA na TPL!
    Ni Zahera ambaye aliitosa timu yake ilipoenda kwa Lipuli eti anaenda jiunga na Timu ya Taifa..Ukweli ni kwamba alienta jiunga na kambi ya AS Vita akitoa siri za Simba iliyomshinda kuifunga.Akapoteza Iringa na Dar pia!Inasemekana aliondoka pamoja na As Vita kwenda DRC!Hatutashangaa akiwapelekea AS Vita Tuyisenge na kuitosa Yanga!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Baadaye anatuambia eti "Boo objectif za Yanga zilikuwa ni kuwa katika 5, 6 na sii chini ya 10 bora na wala si kuchukua kikombe chochote".Huyu kocha ni kigeugeu na nduma kuwili!!Hakumbuki hata alichosema jana

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic