May 12, 2019

UONGOZI wa Yanga umeamua kumfuata moja kwa moja kiungo mshambuliaji wa kikosi cha Kagera Sugar ambaye amekuwa  akiwapa taabu wachezaji wa Simba ambaye pia inasemekana anawindwa na mnyama ili avae jezi yao.

 Kwenye mchezo wa mwanzo uliochezwa Kaitaba alipachika bao la kwanza na mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru ambapo ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 alimsababishai kadi ya njano James Kotei.

Kassim Khamis, mwenye mabao sita kwenye Ligi Kuu Bara ambaye pia uwezo wake umemkosha Kocha Mkuu wa timu ya Taifa kwa sasa saini yake imeelezwa kuwa inawaniwa vikali na vigogo wa soka bongo ikiwa ni pamoja na Simba na Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kassim amesema kuwa kwa msimu huu tangu arejee uwanjani amekuwa akipewa taarifa na meneja wake kwamba kuna viongozi ambao wapo kwenye mazungumzo naye hivyo kwa sasa anasubiri mkataba wake umalizike ndipo ajue jambo la kufanya.

"Nimepewa taarifa na meneja wangu ambaye anasimamia kazi zangu kwamba kuna timu kubwa ambazo zinahitaji saini yangu, ni jambo jema kwangu ila nimemwambia meneja ni lazima nisubiri sina haraka kwa sasa,

"Mwanzo nilikuwa na mazungumzo na Yanga, Alliance, pamoja na Tanzania Prisons hao wote niliwaambia wasubiri kutokana na matatizo ambayo nilipitia ila kwa sasa ninaanza upya," amesema Kassim.

1 COMMENTS:

  1. Huyo kijana akija Dar hana lolote.Akina Salamba wapo wapi? Kwanza sijui hawa vijana wanakwenda kwa waganga ili waoneshe uwezo kwa ajili ya mechi za Simba na Yanga na baada ya hapo hawaonekani kabisa na wakisajiliwa kuja timu hizi za Dara wanaishia kusugua benchi. Simba isifanye masihara katika suala la usajili kwakuwa mchezaji Yanga wanamtaka na wao basi waingie kichwa kichwa. Simba inahitaji viungo waliokamilika kama kweli wanataka kusonga mbele zaidi kimataifa mwakani. Simba waambiwe mara ngapi kuhusiana na mapungufu yaliokuwepo kwenye backline yao pamoja na kiungo? Simba upo ubovu mahali fulani katika watendaji wake kama si kocha mkuu basi kocha wa makipa na kama si kocha wa makipa basi wahusika wanao ahughulikia usajili au management nzima pamoja na benchi la ufundi na wanatakiwa kufanya maamuzi ya kiume ili timu iwe na ufanisi wa maana zaidi. Kufanya kosa kwa mara ya kwanza inahesabika kama ni moja ya njia ya kujifunza lakini kutenda kosa lilelile kwa mara ya pili kwa kweli ni uzembe.Simba inakubali kufungwa na Kagera sugar wanavyojisikia tena Dareslaam? Tena katika mechi muhimu kabisa za ubingwa.Simba inakwenda kupoteza points sita 6 kwa kagera sugar kizembe na kuwapa mdomo kuropoka maneno ya hovyo na wanahaki ya kusema lolote lile juu ya kibonde chao. Hakuna excuse sijui wachezaji wa Simba walikuwa wamechoka au ratiba imewabana tatizo la Simba linajulikana ni timu inayotegemea viungo kama msingi mama wa kuteneza ushindi kwa bahati mbaya sana Simba ya sasa ina viungo hasa wa kati wa kawaida mno na ikitokezea kuzidiwa ujanja kidogo tu katika eneo la kati basi Simba hawana njia mbadala. La kushangaza na kusikitisha tatizo la kuhitajika kwa kiungo hasa mkabaji mwenye nguvu na maarifa zaidi ni suala la muda mrefu.Mwanzoni mwa msimu kulikuwa na tetesi za kumsajili kiungo wa Gormahia ya Kenya Fransis kahata lakini baadae ikaja fahamika kuwa zilikuwa ni habari hewa tu na tangu hapo usajili wa Simba umekuwa ni wa kuuzia magazeti tu na usio wa matendo. Binafsi naiona Simba ikienda kufungwa na Azam fc kwenye mechi ya jumatatu na nafuu waliokuwa nayo Simba ni kwa Yanga kupoteza kule Mara la sivyo hii ngoma bado mbichi kabisa na sijui kwanini Yanga wamevunjika moyo ya nguvu ya ubingwa mapema labda ni janja yao ya kumfanaya Simba abweteke na kwa kiasi fulani walishafanikiwa Yanga kama wangeshinda mechi yao na biashara ya Mara .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic