YANGA HII INATIA SANA HURUMA, HILI NI DONDA
HADI dakika 90 zinamalizika, wachezaji wa Yanga walitoka uwanjani wakiwa hawaamini kitu kufuatia kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Biashara United.
Mchezo huo uliopigwa Dimba la Karume mjini Musoma, ulihudhuriwa na mashabiki kibao wa Biashara United ambao muda wote walikuwa wakiishangilia timu yao hasa ilipokuwa inamiliki mpira.
Biashara kwa sasa inapambana kuhakikisha inabaki ligi kuu kwani kabla ya mechi ya jana ilikuwa nafasi ya tatu kutoka mkiani lakini baada ya ushindi ikakwea hadi nafasi ya 17.
Mechi hiyo ilichezwa huku mvua kubwa ikinyesha kuanzia dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza na kusababisha wachezaji wa timu zote kuteleza na kuanguka mara kwa mara hali iliyopoteza utamu wa soka.
Biashara ilianza kwa kasi mchezo huo ikisaka heshima nyumbani lakini pia kujiondoa kwenye wimbi la kushuka daraja wakati Yanga nao walikuwa hawataki kuona wanaaibishwa na ‘wageni’ kwenye ligi kuu msimu huu.
Bao pekee la Biashara lilifungwa na mchezaji Tariq Seif dakika ya tisa baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Yanga ambao walidhani ameotea kisha akaukwamisha wavuni kiulaini mpira na kumuacha kipa Klaus Kindoki akiangukia kulia na mpira ukaenda kushoto.
Baada ya bao hilo Yanga walijitahidi mara kadhaa kushambulia lango la Biashara lakini mabeki wao walikuwa imara na kuondosha hatari.
Huyu kocha anatakiwa asimamiwe asiachiwe yeye...kusajili wachezaji kwani asije akaleta magharasa lazima alete wachezaji wa hali ya juu...wachezaji wa ndani hao pia wawe wa hali ya juu pia!
ReplyDelete