June 15, 2019

KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Emmanuel Ammunike amesema kuwa kwa sasa kikosi kipo sawa kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Zimbabwe utakaopingwa nchini Misri.

Kwa sasa kikosi cha Stars kipo nchini Misri ambapo kimeweka kambi maalumu ikiwa ni maandalizi kuelekea michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Juni 21 na wameanza kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri.

Amunike amesema kuwa mchezo wa kirafiki waliocheza dhidi ya Misri licha ya kufungwa bao 1-0 umewafumbua macho na kuona mapungufu yao hivyo kuelekea mchezo wa kesho watafanya maajabu.

"Mchezo wetu dhidi ya Misri umetufumbua macho na tumejua mapungufu yetu hivyo tutayafanyia kazi kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Zimbabwe, hii itatufanya tuwe bora zaidi," amesema Amunike.

1 COMMENTS:

  1. Kocha haingiliwi na kuisapoti stars kwa sasa ni lazima kama mtanzania ila sioni kama ni dhambi mtu kutoa maoni yake kutokana na jinsi anavyoona yeye juu ya mustakabali mzima wa timu. Mechi ya Misri, Taifa stars imetumia mbinu ya kujilinda au kupaki basi kuanzia nwanzo wa mchezo mpaka mwisho. Nilitarijia baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila bila kipindi cha pili nilikaa mkao wa kula kuona vijana wetu watakavyofunguka na kuzikonga nyoyo za watanzania lakini lakushanga sikuona mabadiliko yeyote ya kimbinu yaliyofanyika kwa taifa stars wakati wa mapumziko. Wachezaji wa Taifa stars walionekana kuwa waoga wa hali ya juu walikosa kujiamini kabisa. Walishindwa kuanganisha kampa kampa tena angalau pasi mbili.Mara nyingi walishindwa kukaa na mpira na waliupoteza au kupokonywa mpira kirahisi kabisa.Nnaimani kabisa kama mechi ya Taifa stars na Misri ingekuwa ni mechi ya Ngumi japo ya kirafiki basi refa angelisimamisha pambano mapema tu ili kuepusha maafa.Nadhani moja katika ya eneo ambalo taifa stars ilipwaya kabisa ni kiungo nashangaa kwanini Nyoni alikaa nje hakupata nafasi ya kujaribiwa. Ni mechi ya kirafiki hata kocha akibadilisha timu yote kuna tatizo gani.Mimi nitaendelea kupingana na Amunike na benchi lake la ufundi kwa kitendo chao cha kuwadharsu wachezaji wa Simba na nadhani wanafanya kosa kubwa kabisa
    Kwa maoni yangu ya baada samata,msuva,Ulimwengu wachezaji ambao wataendana na kasi ya mashindano yale bila yakuwa na mcheheto wa aina yeyote basi ni wachezaji wa Simba.Katika mechi ya juzi vijana walijitajidi sana kadiri ya uwezo wao kwa maelekezo ya benchi la ufundi nadhani lakini kuna wachezaji walicheza kwakujua nini kinapaswa kufanyika uwanjani bila ya wasi wasi wowote na miongoni mwa wachezaji hao alikuwa shabalala. Hakuonekana kuwa na hofu hata kidogo nilichokiona warabu walianza kuwa na hofu nae. Ya shabalala yanapatikana kwa Manula, Mzamiru, kwa Mkude hata Rashidi Juma. Tunachukulia kimdhaha mdhaha na siasa zetu za usimba na uyanga lakini alipofikia Simba Klabu bingwa Africa Wachezaji wamejifunza mambo mengi juu ya mechi kubwa za ushindani na nnaimani kabisa Kama Waganda wangekuwa na wachezaji sita Simba basi wote wangeliwaita timu yao ya taifa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic