June 23, 2019


KELVIN Yondani juzi alivyoingia tu Instagram alishangaa kuona posti kibao kwenye kurasa za mashabiki wa Yanga zikionyesha beki Ally Ahmed Ally akisaini kuichezea timu hiyo, hapohapo akaguna na kusema “Kwa beki hii? Tafuteni kwa kupitia.”

Yanga mpaka sasa imesaini mabeki wa kati wapya watatu akiwemo Mburundi, Mustapha Suleiyman.

Usajili huo wa mabeki watatu unafikisha idadi ya mabeki watano tofauti na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ anayetajwa kutimkia Ujerumani wengine wawili ni Andrew Vicent ‘Dante’ na Yondani mwenyewe. 

Mabeki wengine wapya waliosajiliwa na Yanga ni Ally Ally aliyekuwa anaichezea KMC ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na Ally Mtoni ‘Sonso’ aliyekuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars.

Akizungumza na Championi Jumamosi kutoka Misri kwenye kambi ya Taifa Stars, Yondani alisema kuwa, usajili huo utaimarisha kikosi chao katika safu ya ulinzi huku akitabiri msimu ujao watakuwa na kikosi kipana na tishio kitakachowapa ubingwa huku akisema sijui wapinzani watapitia wapi?

Yondani alisema, kati ya mabeki wapya waliosajiliwa wote anafahamu uwezo wao, hivyo hana hofu msimu ujao Wanayanga wasubirie furaha kutoka kwao kutokana na maboresho yaliyofanywa na uongozi katika usajili wao.

Aliongeza kuwa, ujio wa mabeki hao wapya hakumpi hofu ya kuondoka kwenye kikosi cha kwanza, kwani anafahamu uwezo wake huku akisisitiza atabaki kuendelea katika kikosi cha kwanza cha Mkongomani, Mwinyi Zahera.

“Ninafurahia maboresho yanayoendelea kufanywa na uongozi katika usajili wao, niwapongeze kwa maboresho makubwa ya kwenye safu ya ulinzi, kiukweli kulikuwa na upungufu mkubwa katika msimu uliopita.

“Lakini nashukuru viongozi wameona upungufu huo kwa kusajili mabeki hao wengine wapya watatu na uzuri kuwa wote tunafahamiana labda huyo mwingine kutoka Burundi lakini Ally na Sonso wote tupo Taifa Stars, licha ya Ally kupunguzwa dakika za mwisho tukiwa kambini Misri.

“Hivyo, msimu ujao utakuwa mzuri kwa timu kuuchukua ubingwa wa ligi na kurejea anga za kimataifa,” alisema Yondani aliyekuwa kwenye kikosi cha stars kitakachojiandaa na Afcon huko Misri.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic