June 23, 2019


Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali ‘Mzee Akilimali’ ambaye ni Katibu ameunga mkono hoja ya Rostam na kusema Yanga haiwezi kumilikiwa na mtu mmoja.

“Kwa kweli mimi nimefurahishwa na kauli ya Rostam na ninamkubali sana kwani klabu kubwa kama Yanga ambayo ina wanachama wengi huwezi kuimilikisha na mtu mmoja kwani kufanya hivyo ina maana kila kitu atakuwa nacho yeye.

“Mimi jana nilimsikiliza mwenyewe na timu kama Yanga inatakiwa iongozwe na wanachama sasa kama mwanachama umeenda pale na kudhani kuwa kuna mdhamini uache kuchangia basi wewe hufahi kuwa mwanachama, mwanachama unatakiwa uchangie."

Kauli ya Akilimali imekuja mara baada ya Rostam kuibuka na kusema anataka kuifadhili Yanga kupitia makampuni yake na si kuimiliki.

5 COMMENTS:

  1. mzee hujitambui mpk xaxa umechangia txhx ngp

    ReplyDelete
  2. Kwani miaka yote mlikuwa wapi au hamkujua kuwa wanachama wanatakiwa kuchangia timu yao?ujamaa na kujitegemea ulisha shindikana kitambo.Tusidanganyane ada ya sh 20,000/= kwa mwaka usitegemee chochote hapo ktk mpira kukua.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiyo elfu 20, hata ukiwa na wanachama million 1 tu, una uhakika wa bill 20 kwa mwaka. Ni club gani tz inatumia bill 20 kuendesha club!? Hata Hugo Mo uwekezaji wake ni bill 20 tu!! Tatizo bongo ni mifumo na wizi!! Ada ya elfu 20 inaweza kuifanya club hapa tz ikatisha sana.

      Delete
  3. Ifike wakati hawa wazee wasipewe Headlines kwenye habari.

    ReplyDelete
  4. Huu wimbo wa kuchangia ada ni sawa na wimbo wa mapambio na umeshasikika miaka nenda rudi lkn hakuna jipya zaidi ya kujipa matumaini kuwa kama tukifanya hivi au kama tungefanya vile tungekusanya bilioni 20 kama ni kitu rahisi hivyo.Mwenye takwimu ya kuwa hizi klabu zetu zina wanachama zaidi ya milioni moja atuwekee hadharani hizo data au atupe mtandao huo uliohakiki.Klabu hizi sidhani hata zimeshafikisha wanachama idadi ya 20,000 na nina uhakika walio wanachama hai si zaidi ya 5,000 na hii inathibitishwa pale wanachama wanapoitisha uchaguzi au mikutano na wanachama hai hujitokeza si zaidi ya 3,000 na mfano halisi ni uchaguzi wa Yanga uliofanyika mwezi mmoja ulioisha, ni wanachama wangapi walijotokeza kupiga kura kuchagua viongozi au ule wa Simba uliochagua viongozi wao mwezi ule wa November?Bila ya mfumo wa mabadiliko na kuturudisha ktk mfumo ule ule wa miaka ilyoanzishwa klabu zetu 1930 kwa kuendelea kuchangishana kwa ada au harambee ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.Huyu mzee Akilimali na kilomoni wameshuhudia hizi klabu zikiendeshwa kwa style hihii.Majengo ya klabu zote mbili yalifadhiliwa na mzee Abeid Karume lkn hakuna mwendelezo wowote tokea miaka ya 1970.
    Tumewaona wafadhili kibao wa Yanga tokea baadhi kama kina Shariff Shiraz,Abbasi Gulamali,Reginald Mengi,Virani(bobby soap), Murtadha Dewji,Manji na Simba kina Ruweh, Azim Dewji, Shaffie, Mo Dewji ( ambaye alijitoa kufadhili na kurejea baada ya Simba kubadili katiba na kuingiza klabu ktk mfumo wa hisa).Kama kweli wanachama wa Simba ambao wanamiliki hisa za kampuni 51% na wamedhamiria kuiendesha kisasa then wangeanza sasa kutafuta mtaji kwa kuwahamasisha wanachama na mashabiki kuchangia kadi mfano wa bank electronic cards za category ya bronze, siver na Gold ili waziingize kwenye mtaji wao wa 51% kwa maana hisa 49% za MO ameshakubali kutoa 20 bilioni hivyo wanachama wasikalie kudokelea 20 bilion ndio zitajengeka uwanja wa mpira kisasa, academy bila kuzalishwa inabidi wanachama wachangamke kwa kutafuta mtaji na 20 biilion ni kama kianzio au kichocheo tu.Nawasilisha hoja nikitegemea marejesho yasikuwa na matusi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic