June 23, 2019


MSIMU ujao wa Ligi Kuu Bara macho na masikio yote yatakuwa kwa washambuliaji, Juma Balinya aliyesaini mkataba wa miaka miwili na Mnyarwanda, Meddie Kagere aliyekuwa mfungaji bora wa msimu uliopita.

Lakini rekodi za Wachezaji hao wawili zinambeba zaidi Balinya ambaye idadi ya penalti kwenye mabao yake ni chache zaidi kuliko Kagere.

Balinya ni kati ya wachezaji nane waliosajiliwa na Yanga hivi karibuni kati ya hao saba wa kigeni na mmoja mzawa ambaye ni kiungo mkabaji, Abdulaziz Makame.

Wengine ni Lamine Moro, Selemani Mustapha, Issa Bigimana, Patrick Sibomana, Maybin Kalengo, Sadney Urikhob na Balinya.

Katika usajili huo unaoendelea, mashabiki wengi wa Simba na Yanga macho na masikio yatakuwa kwa Balinya aliyekuwa mfungaji bora wa Uganda na Kagere aliyekuwa mfungaji bora wa ligi.

Balinya akiwa na Polisi ya Uganda alicheza michezo 24 akafunga mabao 19 na kati ya hayo bao moja pekee ndiyo la penalti. Kagere yeye amecheza michezo 36 akafunga mabao 23 huku mabao penalti yakiwa ni 10.

“Msimu ujao najua timu itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kuna timu nyingi kubwa.

“Huko nimejipanga vilivyo kuona ninafunga zaidi mabao mengi ili nijitangaze mwenyewe lakini niifanye timu ifike mbali zaidi kwenye michuano hiyo,” alisema Balinya Mbali na rekodi hizo, wachezaji kila mmoja amefunga hattrick moja kwenye ligi ya msimu uliopita mpaka anapata kiatu.

Licha ya kwamba Balinya hayuko kwenye kikosi cha Afcon nchini Misri, lakini alihusika kwenye ushindi wa timu yake ambayo ilimaliza kwenye nafasi ya 11 kati ya timu 16.

Kagere ameongezewa mkataba mwingine wa miaka miwili kuitumikia Simba na kufuta ndoto za Zamalek ya Misri ambayo madalali wake walikuwa wakimuwinda.

5 COMMENTS:

  1. Hilo garasa mnataka kulipatia kiki mbele ya Kagere? Thamani ya Kagere ni zaidi ya Dollar laki tatu huyo kanda mbili ana thamani ya kiasi gani? Kamfunika Kagere kwanini kwa shuka? Super wao namba moja waganda Emanueli Okwii kachemsha kwa kagere. Nyie waandishi mnaumwa mavi kweli.

    ReplyDelete
  2. Anafanya nini Dar si timu yake ya Taifa iko Misiri!Acheni kuandika habari za kishabiki..Ukweli ni kwamba alienda kuomba kazi Yanga baada ya kukataliwa Simba... Msimbazi wako makini hawasajili sajili tu!Sadney na Lamine walijaribishwa na wakaonekana hawafai.. HAKUNA MASKAUTI wa kutafuta wachezaji Yanga..ni kuokota alichotema au kubakiza Yanga..kama vile fisi wanapopata riziki kwa akuchoacha Simba mnyama!

    ReplyDelete
  3. Ama kweli wandishi mna vituko na hata mnachoandika ni pumba.Ligi hata haijanza mnaanza kutuandikia utumbo.

    ReplyDelete
  4. Waandishi wengine wana akili za fisi maji!

    Usifute tafadhali!

    ReplyDelete
  5. Waandishi achen bangi huyo kinda ndo mumfananishe na kagere!!!!!!!?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic