FEDHA ZA MAKAMBO KUTOKA HOROYA NI KIZUNGUMKUTI
Imeelezwa kuwa Kaimu katibu mkuu wa klabu ya Yanga, Omary Kaaya ameshindwa kuweka wazi kuhusu malipo ya milioni 230 ya mshambuliaji Heritier Makambo.
Taarifa imesema kuwa Kaya ameshindwa kufunguka ju ya fedha hizo ambazo ni kutoka klabu ya Horoya ya Guinea.
Makambo ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu katika klabu ya Horoya, tayari ameaga Yanga na hatokuwa sehemu ya kikosi msimu ujao.
Mpaka sasa haijawekwa wazi kama fedha hizo zimewasili ama la na tetes za ndani zinaeleza kumekuwa na sintofahamu juu ya uwazi wa kuwasili kwake ndani ya klabu.
Horoya imemchukua mchezaji huyo kutoka Yanga baada ya kumfuatilia kisha kuvutiwa naye kutokana na uwezo wake wa kucheka na nyavu uwanjani
Huyu Kaaya anataka kuwavuruga Yanga....awe makini na hizi kauli
ReplyDeleteZikipotea Tukur wazi tusitegemee kuendelea kupata mchango WA bakuli kwasababu dhana itajengeka kuwa pesa hizo za wala hoyi zinatumbukia katika mifuko ya wajanja na kuwa hapana kuaminiana kama mwenye pumu apate na kikohozi kwahivo shimeni jamaa Mti na jicho tusije tukapoteza kila kitu, amana na imani
ReplyDeleteYanga wawe wawazi tu Makambo alikuwa akicheza yanga kwa mkopo na hakuwa mali yao
ReplyDeleteMbaya sana ni pale ambapo watu hawataki ukweli na kuukumbatia uongo. Makambo alinunuliwa na anamkataba uliosajiliwa wa miaka miwili TFF na sasa kabakiza mwaka mmoja mpaka hapo tupo sawa. Makambo ameuzwa na hiyo hela yaani USD 100,000.00 ni kwa ajili yake na wala si kwa ajili ya Yanga. So ukiconvert in TZS unapata 230,000.00. Makambo hawezi kusign kwa niaba ya Yanga pale alikuwa akisign makubaliano yake na timu husika. Tusubiri uongozi wetu utaweka bayana maana KOCHA amehojiwa na kusema makambo amesajliwa kwa makubaliano zaidi ya mara kumi ya PESA aliyonunuliwa, kitaeleweka tu
ReplyDelete