JIPYA LAIBUKA JUU YA NINJA NA YANGA
INAELEZWA beki wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ anatakiwa na moja kati ya timu zinazoshiriki
Ligi Kuu ya Zambia lakini amepatwa na kigugumzi kufuatia viongozi wa timu hiyo kumtaka kwanza atulie.
Beki huyo amemaliza mkataba na timu hiyo baada ya kujiunga nayo akitokea Taifa Jang’ombe kwa mkataba wa miaka miwili ambapo mpaka sasa licha kudaiwa kupata timu nchini Zambia.
Chanzo cha kuaminika kimeliambia Spoti Xtra beki huyo tayari ana ofa za timu za nje ikiwemo Zambia lakini anashindwa kujua cha kufanya baada ya viongozi wa Yanga viongozi kumzuia kuondoka lakini mpaka sasa hajui kama atapewa mkataba.
Kwa mujibu wa gazeti la Spoti Xtra lilimtafuta Ninja ambaye alisema kuwa: “Niliambiwa nisubirie lakini hadi sasa bado sijapokea simu kutoka kwa viongozi lakini tayari nina ofa kwa timu za nje naweza nikaenda kama nikiona bado wanaendelea kubaki kimya.”
Brother kimbia haraka Yanga hakuna mpango wowote.Subiri ligi ianze utashangaa sana mishahara hakuna
ReplyDeleteHarakisha kabla ya maji kukupwa, wacha Tawi na haraka ukamate Tawi Hamadi kibindoni wasije wakakuliza
ReplyDeleteHiyo ni Subiri ya mnyamwezi WA Pongwe
ReplyDeleteUtakuja Julia uje ujute. Wanaotakiwa wameshachukuliwa na usajili wameshasema umekamilika
ReplyDelete