June 12, 2019

2 COMMENTS:

  1. Jamani msiwadharau wala kuibeza Yanga hii mipango yao na mikakati ya kujiendesha kwa mpango wa muda mfupi, wa kati, na muda mrefu ni mzuri nafikiri njia wanayoitumia Yanga ni njia ya kisayansi zaidi kuliko waliyoitumia Simba....ingawa hatujui na si vizuri kuhukumu iwapo hatujui kiundani ikiwa kwamba kampuni ya Simba Sports Club Ltd imeshaanzishwa na imeshanza kazi au bado.....Tunachokiona na kukishuhudia ni Mwekezaji akiwa mstari wa mbele kuiendesha klabu na timu na mafanikio yake ya muda mfupi yanaonekana kwa timu ya Simba kupata ubingwa na kuingia robo fainali ya michuano ya CAF, mwekezaji huyu pia ana kauli na nguvu kuliko Kampuni inayoitwa Simba Holding Ltd....kuna hiki kinachoitwa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ambapo Mwenyekiti aliyechaguliwa na wajumbe ndiye mwekezaji mwenye 49% ya hisa, wakati klabu ya wanachama ina 51%. Nadhani uwazi na elimu kwa wanachama na wapenzi wa Simba inatakiwa kwa kiwango kikubwa, ili tuone kuwa njia wanayoitumia Simba au Yanga ipi ama ina au/ itakuwa na faida ama tija....katika mitazamo yote miwili Simba yenye mwekezaji na Bodi ya Wakurugenzi na Yanga inayomilikiwa na Wananchi kabla ya kuingia kwenye ubia na mwekezaji ipi ni njia sahihi bila kusahau historia za klabu hizi kongwe katika kuzua migogoro sugu

    ReplyDelete
  2. Angalizo
    Mualike watu watakaoingia na kuichangia Yanga sio tu kuuza sura lengo la kuwepo hapo katika tukio lisisitizwe mara kwa mara kuwa mliopo hapo ni kutoa michango sio kustarehe na kuburudika kwani nimeona wasanii wachezaji wa zamani sijui na wadau wa michezo....mara nyingi matukio kama haya yanapotezaga malengo msipokuwa makini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic