UUONGOZI wa Yanga umesema kuwa, Julai 27 itakuwa ni siku maalumu ya kutambulisha majembe yao mapya pamoja na jezi ambazo watazitumia msimu ujao.
Mpaka sasa Yanga imefanya usajili mkubwa kuliko msimu uliopita jambo linalowapa Imani ya kufanya maajabu msimu ujao wa mwaka 2019/20.
Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa wamezingatia maelekezo ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera hivyo wana Imani ya kuleta ushindani.
Usajili wa beki kiraka kutoka Lipuli ambaye yupo Misri na timu ya Taifa ya Tanzania, Ally Sonso na Farouk Shikhalo ambaye ni mlinda mlango wa Kenya unafanya jumla ya wachezaji 13 wawe wamemwaga wino ndani ya Yanga mpaka sasa.

Sasa nyota hao wawili wanaungana na wachezaji wengine ambao ni pamoja na :Ally Ally maarufu kama mwarabu, beki kiraka ametokea KMC, Patrick Sibomana wa Rwanda, Lamine Moro wa Ghana, Issa Bigirimana wa Rwanda, Maybin Kalego wa Zambia.
Mustapha Suleiman wa Burundi,Juma Balinyi wa Uganda, Sadney Urikhob wa Namibia, Abdulaziz Makame ametoka visiwani Zanzibar, Papy Tshishimbi ameongeza mkataba wa miaka miwili yeye anatokea Congo, Mapinduzi Balama ambaye amejiunga na Yanga akitokea Alliance FC.
Nyie Yanga mtapangaje "Funga Kazi Kusanya Kijiji" ifanyike Taifa kwa Mkapa wakati July 26-28 kwa kalenda ya CAF kutakuwa na mashindano ya CHAN? Hamkuangalia hili? Hamuoni kuwa mtakosa watu au uwanja kuwa na shughuli nyingine ya mchezo baina ya Taifa Stars vs Sudan?? Hebu muwe mnafikiria na kuangalia calendar za Mashindano ya CAF & FIFA Kabla ya kukurupuka na kupata matukio yenye kupanga mkusanyiko mkubwa wa watu....Fanyeni tafiti kabla ya kupanga tarehe za matukio....! Fanyeni haraka kurekebisha hili....hata timu kuingia Kambini tarehe 7 Julai inaweza ikaathiriwa na hili la CHAN
ReplyDelete