June 30, 2019


Uongozi wa klabu ya TP Mazembe ya DR Congo umethibitisha kuwa mshambuliaji wake Deo Kanda yupo nchini Tanzania alipoalikwa na klabu ya Simba kwa mazungumzo ya usajili.

Kanda amewasili Tanzania kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kusajiliwa na tayari kutoa huduma yake kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Mazembe imeingia dili hilo na Simba ambayo pia iliwahi kuwapa mchezaji Mbwana Samatta miaka kadhaa nyuma.

Mbali na Kanda, inaelezwa Simba bado itaendelea kusajili wachezaji wengine wapya tayari kwa kukiweka sawa kikosi kuelekea Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic