NYOTA wa timu ya Taifa ya Uganda na timu ya Simba, Juuko Murshid amesema kuwa yupo fiti kumenyana na Misri bila kuhofia uwepo wa nyota Mohamed Salah anayekipiga Liverpool.
Uganda itamenyana leo na Misri uwanja wa Cairo International ikiwa ni mechi ya mwisho kwenye kundi A ambalo Misri anaongoza akiwa na pointi sita huku Uganda wakiwa na pointi nne nafasi ya pili.
"Tunaamini mechi itakuwa ngumu ila kwenye mpira lolote linaweza kutokea kwa sasa hatuna hofu tupo tayari kupambana," amesema.
Ohh vizuri sana Juuko piga gozi leo wafungeni hao wamisry
ReplyDeletePambaneni vijana ninyi ndio wawakilishi wenye uhakika WA kusonga mbele kuiwakilisha A.Mashariki.
ReplyDeleteJuuko? Walahi kama angekuwa Mtanzaia basi zamani sana kesha stahafu mpira. Sisi watanzania ni watu wa ajabu sana.Tatizo la Juuko Simba linachangiwa kwa kiasi kikubwa na wao wenyewe Simba kumtoa mchezoni. Wanachotakiwa kufanya Simba ni kumuamini Juuko kwenye kazi yake uwanjani kwa asilimia mia moja basi wakifanya hivyo Simba watampata yule Juuko wanaemuona ndani ya timu ya Taifa ya Uganda.Sio akifanya kosa moja watu wote wanaanza kutapika. Hali hiyo ni rahisi kumfanya mchezaji kuingiwa na hali ya kutojiamini uwanjani.Waganda hawana mashaka na ufanisi wa Juuko hata kidogo. Na ndani ya timu ya Taifa Uganda kuna ushindani wa kweli wa namba lakini kila kocha anaishika mikoba ya the crane kuanzia Mserbia na sasa Mfaransa wamekuwa hawana mashaka na Juuko.kweli Juuko huwa anacheza kazi lakini kwa beki wa kati vitu hivyo ni mambo ya kawaida.Angalia Ramosi wa Madrid akimaliza mechi tatu bila kadi basi ni kitu cha ajabu lakini ni miongoni mwa mabeki bora wa kati Duniani. Pale Simba Juuko alianza kufanyiwa figisu zamani sana.Na Simba walifanya hivyo kwa Kevin Yondani na matokeo yake wameyaona. Juuko na wawa basi Juuko ni bora mara nyingi sana na itakuwa kichekesho kama Simba watakubali kuruhusu Juuko aondoke halafu wawa abaki.Ninaimani hata kocha wa Simba huko aliko akiangalia Afcon kama alikuwa na mawazo ya kumuondosha juuko basi lazima atajiuliza tena.
ReplyDeleteKweli umesema brother
Delete