June 13, 2019


ANAFICHA mimba! Ndivyo walivyosikika mashabiki waliomuona mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch kutokana na kuwa na tumbo kubwa hivyo kuibua gumzo kama lote kuwa ni mjamzito.

Mara kadhaa Tanasha amekuwa na kigugumizi juu ya suala la kuwa na mimba ya Diamond akisisitiza muda ukifika ataweka wazi.

Ishu hiyo iliibua gumzo kwa mara nyingine wikiendi iliyopita baada ya mrembo huyo kunaswa akicheza muziki na kunywa akiwa na Diamond katika kiwanja cha bata ndefu cha Ultra Gossip Lounge kwenye Majengo ya Lavington Mall jijini Nairobi, Kenya.

Mara tu baada ya kumuona, mashabiki hao mara moja walitoa simu janja zao na kuanza kurekodi video huku wakipiga kelele; “Anaficha mimba!”

Muda mfupi baadaye, video za tukio hilo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha Tanasha akijitahidi kuficha tumbo lake ambalo lilionekana kuwa ni kubwa.

Mapema mwezi Aprili, mwaka huu, wakati akifanyiwa mahojiano na redio moja jijini Dar, Tanasha aligoma kusema chochote juu ya tetesi hizo kuwa ana mimba ya Diamond ambapo aliishia kusema; “Muda utasema.”

Hata hivyo, katika moja ya posti zake kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram, Tanasha aliacha maswali mengi baada ya kudai kuwa anatarajia kupata baraka kubwa mno kwenye maisha yake ambapo bila kupepesa macho, watu waliunganisha nukta na kusema baraka hiyo ni mtoto wake wa kwanza atakayemzalia jamaa huyo.

“Jambo kubwa kwenye maisha yangu ni kwamba ninatarajia baraka kubwa hivi karibuni. Mungu ni mwema,” aliandika Tanasha bila kusema ni baraka gani hasa. Kwa wale wanaomfuatilia Tanasha kwenye ukurasa wake wa Instagram, hivi karibuni amekuwa akiposti picha za zamani tu, jambo ambalo limekuwa likiongeza mashiko kwenye tetesi hizo za kuwa ni mjamzito.

“Hivi ndivyo inavyokuwa mwili unapoanza kubadilika na uzito kuanza kuongezeka,” aliandika mwanadada huyo ambaye ni muuza sura kwenye video za wasanii, mwanamuziki na mtangazaji wa Kituo cha Redio NRG cha Mombasa, Kenya.

Wiki iliyopita, gazeti pendwa ndugu na hili, Amani linalotoka kila Alhamisi lilimtafuta Tanasha na kumbana juu ya mambo mbalimbali likiwemo suala hilo la kuwa mjamzito ambapo alijibu; “Napenda kuwaambia watu wasiamini kila wanachokiona kwenye mitandao ya kijamii hasa kwenye hizi kurasa za udaku na umbeya.”

Tukio la Tanasha kunaswa na kitumbo hicho kikubwa liliambatana na uzinduzi rasmi wa video ya Wimbo wa Inama wa Diamond aliomshirikisha mwanamuziki Fally Ipupa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ndani ya saa 16 tu baada ya kuzinduliwa Juni 9, video hiyo ilikuwa ina watazamaji (views) milioni moja kwenye Mtandao wa YouTube.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic