June 6, 2019


Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amefunguka kwa kutoa rai kwa viongozi wa klabu hiyo juu ya usajili wanaoufanya hivi sasa.

Mkwasa ambaye hivi sasa bado anaugulia kutokana na tatizo la moyo lililomfanya aachie ngazi Yanga, ameamua kuweka wazi suala la usajili unaondelea klabuni hapo ambao unaenda kwa kasi.

Mkwasa amesema ni vizuri zaidi Yanga wakaangalia wachezaji ambao watakuwa na msaada ndani ya timu.

Amesema si vema kusajili wachezaji kupitia 'KLIPU' za YouTube maana haziamini na wengi kuwa wanazitengeneza.

"Ni vizuri Yanga wakasajili kwa kuangalizia vipaji na si YouTube.

"Klipu nyingi za YouTube zinakuwa ni za kutengenezwa hivyo ni vema wakawa makini zaidi."

4 COMMENTS:

  1. Duh lakini Mkwasa si mapendekezo ya kocha au ya viongozi?Tuelewashane

    ReplyDelete
  2. nadhani issue ni uendelevu wa hao wachezaji hasa suala la marupurupu

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana sana na Mkwawa huu mtindo kiutalaamu sio mzuri

    ReplyDelete
    Replies
    1. mpaka sasa hakuna mchezaji aliyesajiliwa kupitia you tube......wachezaji wote ni mapendekezo ya kocha kwakuwa alishawafahamu kitambo.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic