June 29, 2019

IMEELEZWA kuwa Yanga kwa sasa hawataki utani kwani wamedhamiria kujenga kikosi imara kitakachorejesha furaha Jangwani hali iliyofanya wasajili nyota wakali.

Miongoni mwa nyota ambao wamesajiliwa ndani ya Yanga ni pamoja na Juma Balinya, Aly Ally, Maybin Kalengo,Issa Sibomana na Patrick Bigirimana inawafanya waachan na nyota wengine ndani ya kikosi hicho.

Usajili wa Yanga ambao umetikisa unampa kiburi Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ambaye ameshika hatma ya nyota wa Yanga hivyo hata ya nyota wake nane ameishikilia yeye.

Habari kutoka ndani zimeeleza kuwa wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga ambao wanasubiri kujua hatma yao ni pamoja na :-

Ibrahim Ajibu.

Thaban Kamusoko.

Amiss Tambwe.

Pius Buswita.

Mwinyi Haji.

Abdalah Shaibu.

Said Juma.

Mrisho Ngasa.


4 COMMENTS:

  1. Amiss Tambwe Kwa hivi karibumi anmekuwa akiisifu na kuigombania sana Yanga kwahivo naona aonewe huruma nahisi akitupwa haitokuwa rahisi kwake kupata timu nae aliinyanyuwa Sana yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aende pale Azam maana kocha anawebeba sana warundi wenzake

      Delete
  2. Tatizo linakuwa nini kwa wachezaji wetu wa kitanzania? Hawajitambui na maisha yao ya baadaye au wanacheza soka as a pleasure? Nasikitikia kipaji kama cha kina Pius Buswita,Saidi Makapu,Pato Ngonyani,Mohammed Rashid,Salamba,Danny Lyanga,Peter Manyika,Jamal Mwambeleko,Kaheza,na wengineo wengi wameshapotea mapema sana.Ushauri wangu wasiwe na papara ya kuchezea klabu kubwa za Simba,Yanga na hata Azam ambao nao wako kwenye siasa za Simba /Yanga bali wawe wanajijenga na timu za kawaida kama walivyofanya kina Eliud Ambokile (TP Mazembe),Habibu Kiyombo( Mamelod Sundowns) Salim Ngazi (USA)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kacheza hajapote wala mwambeleko na manyika wapo kenya

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic