MSHAMBULIAJI wa timu ya Kagera Sugar, Kassim Khamis ambaye aliitwa timu ya Taifa kikosi cha awali na kuachwa dakika za lala salama wakati kikosi kinapaa kwenda Misri amesema kuwa ni wakati wa kuiombea timu kufanya maajabu nchini Misri.
Akizungumza na Salehe Jembe, Kassim amesema kuwa kuitwa kwake ndani ya kikosi cha Taifa ni sehemu ya ndoto zake hata kuachwa kwake ni sehemu ya mchezo.
"Taifa lina wachezaji wengi wazuri achilia mbali idadi ya timu, kuwa sehemu ya kikosi cha awali si kitu chepesi hivyo kuachwa pia ni sehemu ya mchezo, bado ninaipenda timu yangu ya Taifa na ninawaombea kheri huko Misri.
"Imani yangu kila kitu kitakuwa sawa na watafanya maajabu kwa kuwa Taifa linawategema na tunawaombea huko waliko," amesema Khamis.
Stars imeweka kambi nchini Misri ikiwa ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Juni 21.

0 COMMENTS:
Post a Comment