Chirwa ameigomea Azam FC kuongeza kandarasi nyingine baada ya mkataba wake wa awali kufika tamati hali iliyofanya viongozi kumuweka kando kwa muda.
Akizungumza na Salehe Jembe, Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa kwa sasa hawafikirii suala la wachezaji kwa kuwa sio kipaumbele chao kikubwa sana muda huu.
"Kwa sasa hesabu zetu sio kwa wachezaji hilo la wachezaji ngoja tuliache kidogo baada ya muda tutarudi tu kwani hakuna kinachoshindikana subiri kwanza tumalize suala la mwalimu.
"Tumeweka nguvu kubwa kwanza kwa mwalimu kisha tukishakamilisha suala la mwalimu hapo masuala ya wachezaji yatafuata, kuanza kesho tutakuwa na taarifa mpya, hivi karibuni," amesema Alando.
0 COMMENTS:
Post a Comment