June 15, 2019


KAMA mipango ikienda sawa huenda nyota wa Simba, Adam Salamba akatua Afrika Kusini kukipiga klabu ya Polokwane FC.

Dili hilo limekuja baada ya dili la mshambuliaji John Bocco kuingia doa kwa kile kilichoelezwa kwamba Polokwane FC walimsainisha mchezaji kimakosa hivyo wameamua waikomalie Simba iwape mchezaji mmoja kwa mkopo.

Uongozi wa Simba kupitia Mtendaji Mkuu, Cresesteus  Magori umesema kuwa kumtoa Bocco ni ngumu hasa kutokana na malengo ya klabu ya Simba kwa sasa kuwa ya kimataifa.

"Kumtoa mchezaji kama Bocco kwa sasa ni ngumu hasa ukizingatia Simba ni timu kubwa hivyo kumpeleka Afrika Kusini bado sio sahihi, hilo limeisha na viongozi wa Polokwane wameelewa na kwa sasa wanahitaji mchezaji wetu mmoja kwa mkopo," amesema.

Mchezaji huyo ambaye Polokwane wamemuomba imeelezwa kwamba ni Adam Salamba. 

2 COMMENTS:

  1. Wapeni lakini wasiwe wagumu kumrejesha pale muda wa mkopo kumalizika na huku wenyewe Simba wakimjitajia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic