June 5, 2019


Kwenye ripoti ya usajili wa Simba ambayo imeachwa na kocha wao Patrick Aussems, amewataka vigogo hao kusajili beki mmoja wa kati kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa Jumamosi iliyopita mabosi wa Simba walikutana na wakala Patrick Gakumba kwa ajili ya kumalizana kuhusiana na beki Ange Baresi Gloudoueu ambaye ni raia wa Ivory Coast.

Mabosi hao wa Simba walikutana na Gakumba ambaye yupo nchini na akiwa amefikia kwenye moja ya hoteli zilizopo Kariakoo kwa ajili ya kumsajili Gloudoueu ambaye ana uzoefu mkubwa na michuano ya kimataifa.

Beki huyo ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, anapigiwa hesabu kali na Simba ili kuja kuongeza nguvu katika kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Taarifa zinaeleza kwamba mabosi wa Simba walikutana na Gakumba juzi Jumamosi na kuzungumza namna ya kumalizana na Gloudoueu.

“Ndiyo ni kweli, viongozi wa Simba na Gakumba walikutana juzi (Jumamosi) na kuzungumza naye.

“Mabosi hao wakiongozwa na Mtendaji Mkuu (Crescentius Magori) walizungumza naye juu ya usajili huo na muda siyo mrefu huenda beki huyo sambamba na wachezaji wengine watatu wakaja Simba kwa ajili ya kumalizana na uongozi,” kilisema chanzo hicho.

Ikumbukwe kuwa Gakumba ndiye ambaye amemleta nchini straika Meddie Kagere kutoka Gor Mahia na kumsainisha mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo.

3 COMMENTS:

  1. Mambo kimyakimya bila ya kelele ndivo alivo Mnyama

    ReplyDelete
  2. HUYU MCHEZAJI HATUFAI TUJENGE TIMU YA MUDA MREFU. MCHEZAJI WA MIAKA 32 HATUFAI MTU ANACHEZA TANGU 2005 MPAKA LEO 2019 USITEGEMEE KUWA FITI KWA ASILIMIA 80.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic