June 23, 2019


ROSTAM Aziz ni kama mfalme kwa sasa Yanga hii ni baada ya mastaa wa zamani wa Yanga, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ na Sekilojo Chambua kuupongeza ushauri alioutoa kwa klabu hiyo.

Juzi Alhamisi, Rostam alijitokeza hadharani na kuweka wazi mikakati yake ya jinsi gani ataisaidia Yanga ili iweze kutoka hapa ilipo na kupiga hatua kubwa kiuchumi kama zilivyo klabu nyingine kubwa Barani Afrika.

Rostam ambaye alichangia Sh mil 200 kwenye harambee ya Kubwa Kuliko ambayo iliandaliwa na klabu hiyo Jumamosi iliyopita, alisema ataisadia Yanga kama mpenzi na shabiki wa timu hiyo lakini siyo kama mfadhili au mmiliki.

Hali hiyo imepokelewa kwa mikono miwili na wapenzi na mashabiki wa Yanga kwa kudai kuwa itaifanya Yanga kuwa kubwa na ambayo itakuwa ikijiendesha yenyewe pasipo kumtegemea mtu mmoja Wakizungumza na Championi Jumamosi, Chambua na Jembe Ulaya walisema Rostam ametua Yanga kwa wakati muafaka hivyo sasa Yanga itapiga hatua kubwa zaidi kisoka.

“Rostam amekuja katika kipindi ambacho tunaamini kuwa atakuwa na msaada mkubwa kwa Yanga katika kuhakikisha inapiga hatua zaidi kiuchumi pasipo kumtegemea mtu mmoja au mfadhili. “Lakini pia mfumo wake wa kutaka kuiona Yanga ikiendelea kuwa chini ya wanachama kwa asilimia 100 utaisaidia kuifanya timu kuendelea kuwa karibu kabisa na wanachama wake kama ilivyo zamani.

“Kwa hiyo mpaka anafikia hatua ya kusema hivyo na kuhaidi kuwa yupo tayari kwa hali na mali kuisaidia Yanga ili iweze kuwa katika mfumo bora wa kujiendesha yenyewe kuna jambo ameliona, binafsi namuunga mkono katika hilo na ninamkaribisha Yanga kwa ajili ya kuwa mdhamini na siyo mfadhili wala mmiliki,” alisema Malima. Naye nahodha wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua alisema: “Mfumo ambao Rostam amekuja nao ni mzuri. Pia utapunguza migogoro kama ambayo hivi sasa tumekuwa tukiisikia huko upande wa pili.”

“Kikubwa inatakiwa tu kufanyike marekebisho ya katiba yetu na kuweka vifungu ambavyo vitatusaidia katika kuhakikisha mipango hiyo ya Rostam ya kuruhusu wadhamini wengi kuja kudhamini timu yetu inatekelezeka bila ya kuwepo kwa vikwazo vyovyote.”




2 COMMENTS:

  1. Ebu tusubiri ligi ianze na baada ya miezi 3 uje uwaulize tena hao kwamba mfumo bora ni upi

    ReplyDelete
  2. Watanzania akili zetu zimejikita zaidi katika kupata vitu vya bure.
    Yanga haiwezi kufika mbali kwa aina hii ya kujiendesha.Na ukiangalia sana kinachoendelea ndani ya Yanga ni kamapeni za kijinga za kuonesha kana kwamba Simba wamekosea kuamua kujiendesha kwa mfumo wa hisa.Ila Simba wameamua kitu cha kipekee kabisa kwa maendeleo halisi na ukombozi wa maendeleo ya mpira nchini na wanastahiki pongezi Kuna watu wanachuki zao binafsi na Mo unaweza kusema ni wivu. Mo akitoa pesa Simba hatoi bure na kama ataamua kutoa bure sawa ila Mo ni partnership na mdau mkuu wa kuwaongoza wanachama wa Simba kufikia malengo ya klabu yao.
    Kuna watu kamwe wasingependa kuiona Simba ikijitofautisha kimaendeleo.Wivu wa baadhi ya watu Yanga kwa maendeleo ya Simba wakati mwengine unavuka mipaka hadi kufikia kiwango cha uchawi.Kiukweli Yanga ni timu iliyofeli choka mbaya katika kipindi hiki cha mageuzi ya kimaendeleo nchini lakini katika kuficha uchafu wao wanaendesha kampeni za kijinga ionekane kana kwamba Simba ndio timu inayopoteza muelekeo kimaendeleo.Mo na uongozi wake wapo pale Simba kisheria kwa baraka za wapenzi na wanachama wa Simba.Nashangaa kusikia baadhi ya viongozi wa siasa au viongozi wastaafu wa mpira nchini wakikosoa mabadiliko ya uendeshaji ndani ya Simba. Yaliyofanyika ndani ya Simba ni maamuzi ya kidemokrasia ya watu wa Simba yaliyofanyika hadharani na wengi ya wanachama wakapitisha maamuzi ya kujiendesha kisasa zaidi.Wewe unaehoji au kupinga ni kama nani kwa nini ushindwe kuheshimu maamuzi ya wengi. Hata Edward Lowasa alinuna na kupinga mageuzi ndani ya CCM lakini kamwe mtu au kikundi cha watu hakiwezi kushindana na nguvu ya umma iliowengi utaishia pabaya tu. Simba ipo kwenye mfumo wa kimaandishi kwa maana ya kwamba ya kuainisha mapato na matumizi ya klabu pamoja na kuziainisha mali zake zote zijulikane kisheria na ziwe chini ya Simba na nadhani hapo ndipo panapoleta fukuto na msuguano ndani ya Simba kwa baadhi ya watu au viongozi wanaojifanya kuwa wao ni wanasimba wa milele wasiotaka mabadiliko lakini kiukweli hao ndio watu walioiibia Simba sana na wanaoendelea kuibia Simba hadi leo kwa kutumia mali za Simba.
    Leo hii Mo anachokitoa kwa ajili ya klabu kinakwenda moja kwa moja kwenye maendeleo ya klabu ya Simba kwanini Simba isipae juu kwa kasi ya ajabu kimaendeleo? Wanachama na wapenzi wa Simba wanatakiwa kushikamana zaidi na kuzidi kumpa sapoti ya nguvu ya hali na mali Mohamedi Mo na uongozi wake na kupuuza maneno ya kifitina juu yake. Magufuli katika Ubora wake kwenye kauli yake iliyopaswa maneno yake kuandikwa kwa wino wa dhahabu,alisema. Nanukuu...Nchi hii ukiona kiongozi fulani wa umma anapigwa vita basi ujue huyo kiongozi anatimiza majukumu yake ya kuwatumukia wananchi na taasisi anayoiongoza ipasavyo. Mwisho wa kunukuu. Miaka kadhaa Simba iliyoshindwa kupiga hatua lakini kuna watu wasingependa kuiona Simba ikipiga hatua za haraka za kimaendeleo chini ya Mo. Kuna watu wanahofu labda Mo anaweza kuja kuonesha mazaifu ya baadhi ya viongozi waliopita. Kuna wanasiasa vile vile wasingependa kuona awamu hii ya tano kila kitu kinawezekana na moja ya sekta iliyokuwa imeoza kabisa ni sekta ya michezo. Agizo la Muheshimiwa Raisi kwa Simba mwaka Jana kwa kiasi fulani Simba wametimiza wajibu wao. Na licha ya viji neno neno kwa ninavyomtambua Magufuli najua anaziona juhudi za Simba katika kuinua kiwango cha mpira nchini na anafuatilia kwa karibu zaidi na wenye kupiga majungu basi waache kupiga majungu na kama Yanga wameamua kujitofautisha kiundeshaji basi ni nzuri zaidi kwani kutakuwa na ushindani wa kimaendeleo pia kuangalia mfumo upi wenye tija zaidi kwa maendeleo ya Klabu ila nadhani kama Yanga wangejiweka kihisa basi wangeuza hisa zao kisheria kwa wanachama wao badala ya kukusanya michango na haijulikani inaishia wapi Kwa Simba gari limeshawaka kama Standard Gauge ya Magufuli hakuna kurudi nyuma.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic