SIMBA WAAMUA KUIIGA YANGA KWA JAMBO HILI
Klabu ya Simba imetangaza rasmi kuandaa mchakato wa kupata wimbo wake maalum kwaajili ya mashabiki kama sehemu ya kuongeza hamasa.
Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Crescentius Magori amesema wimbo huo utakuwa tayari kabla ya kuanza kwa wiki ya Simba mwezi Agosti mwaka huu hivyo watakaribisha tungo mbalimbali kutoka kwa wasanii.
Amesema mchakato huo utasimamiwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba Haji Manara na siku chache zijazo wasanii watatangaziwa hatua za kufuata ili kuwasilisha kazi zao zitakazoshindanishwa ili kupata wimbo mmoja.
Ikumbukwe takribani misimu miwili nyuma Yanga walitangaza kuandaa wimbo maalum ambao utakuwa unatumika katika shughuli zao mbalimbali ikwemo kwa mashabiki kuuimba uwanjani ingawa mpaka sasa bado haujatambulishwa rasmi.
Sasa Simba wameiga Yanga katika lipi wakati wao wenyewe Yanga hawana wimbo wa timu? Uandishi wengine hovyo kabisa .
ReplyDelete