KAMA zali tu vifaa vipya ambavyo vitavaa jezi za Yanga msimu ujao vina nafasi kubwa ya kukipiga dhidi ya timu za TP Mazembe na Al Ahly, hiyo ni baada ya wapinzani wao Simba kuwakutanisha na timu hizo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Yanga kupata nafasi ya kushiriki katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwa msimu ujao watacheza huko baada ya kupata nafasi kutoka kwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
Taarifa rasmi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyotolewa jana Jumanne imeeleza kuwa Yanga wamepata nafasi hiyo baada ya kuongezwa kwa timu za Tanzania katika michuano ya kimataifa iliyo chini ya Caf kutokana na mafanikio ya Simba msimu uliopita wa 2018/19.
TFF imeeleza kuwa timu mbili zitawakilisha Ligi ya Mabingwa Afrika na mbili nyingine zitashiriki katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho imekwenda kwa Azam FC ambao ni mabingwa wa Kombe la FA na Timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) ambao wenyewe wamepata nafasi hiyo ya upendeleo kwa kuwa walishika nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa kutokana na Simba kufika hatua ya robo fainali msimu uliopita, kumeifanya Tanzania kufikia vigezo vya CAF katika kupanda ubora wa kiwango cha nchi upande wa klabu na kufikia nafasi ya 12 kwenye viwango vya ubora.
Tayari CAF imefungua dirisha kwa mashirikisho kusajili timu kupitia mtandao wa CMS, mwisho wa kufanya hivyo ni Juni 30, mwaka huu. Rais wa TFF, Wallance Karia amezitaka timu zilizopata nafasi kusajili kwa umakini ili kujiandaa na mshindano hayo kulinda nafasi nne kwenye michuano ya CAF.
Daah mshikaji unaandika utumbo hata haueleweki
ReplyDeleteUse your brain to write such news for the public! The reason why yanga and KMC are going in is not because ONLY simba went through quater final but it is because of overall 5 years collective points accumulated by Yanga and Simba!,TUMIENI AKILI MNAPOANDIKA HIZI NEWS BECAUSE WASOMAJI NI WENGI SANA
ReplyDeletesasa ukiandika kiingereza ndio tuone umeelewa sana mbona nyi watu mnakuwa mambumbumbu hivi?hebu fafanua yanga wamechangia point ngapi na simba point ngapi sio kuila jambo kubishabisha tu nyie vyura wa matopeni...........hiyo nafasi mliyopata bila simba msimu uliopita kufika robo mungeipata?acheni ubishi nyie washiriki wa viti maalumu au waalikwa...maana simba bado wangeendelea kushiriki kama mabingwa wa nchi na azam wangeshiriki kama mabingwa wa FA je nyinyi na kmc mnashiriki kwa vigezo gani?nyambaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaf
Deleteacha ujinga! miaka mitatu Yanga alikuwa anacheza ubingwa mbona mshinda wa pili au Simba au Azam haukuchea CAF!miaka mitatu point tatu...Simba mwaka mmoja point 12!Yanga wakubali tu!wasingecheza CAF kama sio Simba!Na ni fadhila wanazozipata pamoja na kuwa walikuwa wanaenda uwanja wa Taifa kushabikia NKANA na TP Mazembe.
DeleteElite my block this site if you don't write comprehensive and true stories.
ReplyDelete