UONGOZI SIMBA WATOA TAMKO JUU YA YANGA KUWA MOJA YA TIMU SHIRIKI CAF MSIMU UJAO
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi katika klabu ya Simba, Salim Abdallah 'Tyry Again' amesema ni faraja kubwa kwa Tanzania kupata timu nne zitakazoshiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao ikiwemo Yanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) jana, ilisema kuwa Simba na Yanga zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika huku Azam na KMC zitacheza Kombe la Shirikisho.
Again ameeleza kuwa ni jambo kwa watanzania kupata ongezeko la timu kwani itakuwa inaitangaza vizuri nchi.
Amefunguka kwa kusema kinachopaswa kufanyika hivi sasa ni mapambano zaidi yanapaswa kuanza kuelekea kwenye mashindano hayo.
"Ni jambo la faraja, timu zimeongezeka na sasa tuna wajibu kwa kujipanga vizuri.
"Kinachopaswa ni kufanya maandalizi ili kwenda kupambana zaidi kwenye michuano."
0 COMMENTS:
Post a Comment