June 4, 2019

BEKI kisiki wa Simba mwenye mwili uliojengeka kimazoezi Pascal Wawa amesema kuwa kwa sasa anatarajia kuondoka bongo muda wowote kuelekea nchini Ivory Coast kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa baada ya kutwaa ubingwa ndani ya kikosi cha Simba ni muda mwafaka kwake kusepa kwenda nyumbani kupumzika ili kujiandaa kwa msimu ujao.

"Nashukuru, kwa kushirikiana na wenzangu tumebeba ubingwa hilo lilikuwa ni jambo kubwa na la msingi, kilichobaki kwa sasa ni kuondoka kurejea nyumbani kuiona familia yangu.

"Sitakaa sana hapa bongo inanibidi niondoke kwa kuwa nilikuwa ninamajukumu namalizia ila kwa sasa nitaondoka kwa ajili ya kupumzika," amesema Wawa ambaye amecheza jumla ya michezo 21 ndani ya Simba.

3 COMMENTS:

  1. Kweli, tena sio ukakasi mdogo! Kwa haraka haraka, headline inatoa picha kwamba 'anaondoka' kbs! Nadhani mwandishi kawa mvivu kdg,kuna 'gaps' kadhaa kwy habari hii hakuzijaza...na hivyo kutuacha wasomaji na maswali mawili matatu!

    ReplyDelete
  2. mwandishi kanjanja katika ubora wake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic